Habari/News

Hii ndiyo sababu Mbatia kuvunjika Mkono

Tarehe December 21, 2017

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia

Sababu iliyopelekea Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia kuvunjika mkono imetajwa kuwa ni kuteleza na kuanguka wakati akiondoka hotelini kurejea nyumbani.

Kwa mujibu wa Msaidizi wa mbunge huyo, Hamis Hamis alisema jana Jumatano Desemba 20,2017 kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 2:45 usiku wakati akiondoka hotelini kurejea nyumbani.

Hamis alisema Mbatia alikuwa akishuka ngazi katika hoteli ya Uhuru iliyopo eneo la Shanty Town ndipo alipoteleza na kuanguka na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi.

“Bahati nzuri pale kulikuwa na daktari wa KCMC anaitwa Ansbert Sweetbert ndiye alitoa huduma ya kwanza hadi kumpeleka KCMC,” alisema.

Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amevunjika mkono wa kushoto  amelazwa katika wodi za watu mashuhuri (VIP).

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni