Habari/News

Hii ndiyo mikoa minne Kinara kwa Utoro wa wanafunzi

Tarehe April 2, 2018

Wanafunzi katika moja ya shule ya sekondari nchini.

Serikali imeitaja   mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa sekondari hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa ambapo ameitaja pia mikoa ya Rukwa, Geita, Tabora, Singida na Simiyu kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi.

Aidha, amesema Mkoa wa Tabora unaongoza kwa asilimia 9.7 ya wanafunzi watoro wa sekondari ukifuatiwa na Geita (asilimia 8.1), Mtwara (asilimia 6.1) na Shinyanga (asilimia 6.3).

Kwa shule za msingi, Rukwa inaongoza kwa asilimia 3.2, ukifuata Geita (asilimia 3.1), Tabora (asilimia 2.9), Singida (asilimia 2) na Simiyu (asilimia 2).

Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumatatu Aprili 2,2018 wakati akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Magogo mkoani Geita.

Mbio za Mwenge zimeanza leo na zitakahitimishwa Oktoba 14,2018 mkoani Tanga.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru kwa huu ni  “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya nchi yetu.”

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni