Tarehe February 2, 2018

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru enzi ya uhai wake.
Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Februari 5, 2018 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia msiba huo Mwenyekiti wa kamati ya maziko ya mwanasiasa huyo, Omary Kimbau amesema Kingunge atazikwa saa tisa alasiri.
Amesema leo Ijumaa Februari 2,2018 kuwa utaratibu na mipango mingine inaendelea kufanyika.
Kingunge ambaye ni mwanasiasa Mkonge na Mwasisi wa Chama cha Mapinduzi amefariki dunia leo alfajiri akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Alikuwa akiuguza majeraha baada ya kung’atwa na mbwa mwishoni mwa mwaka jana nyumbani kwake.
Mpwa wa Kingunge, Tony Mwiru amesema familia inapitia kipindi kigumu kwa kuwa hivi karibuni wamempoteza mama yao, Peras.
Maoni