Habari/News

Halima Mdee akamatwa na Polisi ‘Airport’,Chadema yatoa neno

Tarehe April 1, 2018

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee akamatwa na Polisi leo.

 

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar, katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.

Mdee amekamatwa alipowasili majira ya saa 9 alfajiri, akitokea nchini Afrika Kusini, ilikoelezwa kuwa alikuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa ambao haujawekwa wazi.

Uamuzi wa Jeshi la Polisi kumkamata  Mdee unafuatia  Halima Mdee na Mwenyekiti Freeman Mbowe kutakiwa kuripoti Polisi  kwa amri ya DCI ambapo Jumanne tarehe 27 Machi hakufika kutokana na kwenda nje ya nchi kwa matibabu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema
“Halima Mdee bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi wa kituo cha ‘Centro’ Jijini Dar es Salaam mpaka hivi sasa japokuwa amewaeleza ukweli kwamba ametoka kwenye matibabu na kuwaonesha vyeti vyote vya hospitali lakini bado wanaendelea kumshikiria”

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni