Habari/News

Gambo atema cheche kuhusu wanawake aina ya ‘Bebi nina njaa’

Tarehe February 26, 2018

 

Mrisho Gambo mkuu wa mkoa Arusha.

Wakati baadhi ya wanawake wakiendekeza tabia  ya kuwafanya wanaume kuwa kitega uchumi,Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wanaume kuachana na wanawake wa aina hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa  mitandao ya kijamii Gambo amesema kuna rundo la wanawake ambao kazi yao kubwa ni kutafuna pesa za wanaume  katika starehe na sio kuwashauri ni namna gani wafanye wajikwamue katika maisha hasa ya sasa ambayo wengi wao wanasema yamekuwa magumu.

“Mwanaume Kama unania ya dhati kuwa na ‘economic freedom in this tough economy’ basi inatakiwa uepukane na wale wanawake aina ya ‘Babe’ nina njaa, nibebee Pizza au Chips kuku usisahau kuweka ‘mayonaise’ au ‘Babe’ simu Iphone X imetoka naomba ninunulie”, amesema Gambo.

Gambo amesema wanaume wanapaswa kuacha kuwa na mahusiano na wanawake wasiokuwa na mawazo ya kupambana na hali ya uchumi wa maisha na badala yake kutaka kula starehe peke yake bila ya kujali kesho yao.

“Spidi ya mwanaume kuwa na maendeleo na hatimae kushinda uhuru wa kiuchumi inategemeana sana na aina ya mwanamke uliyenae. Mwanamke bora ni uwekezaji wenye faida kubwa na mwanamke asiejua nafasi yake ni mzigo na ‘liability’ kubwa sana”.Ameongeza Gambo

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni