Habari/News

Familia yatoa neno jina la Lowassa kuibuka kwa Makonda

Tarehe April 11, 2018

Fred Lowassa,mtoto wa Mwanasiasa Edward Lowassa.

Mtoto wa Lowassa anayejulikana kwa jina la Fred Lowassa ameonesha kusikitishwa na kitendo cha mama mmoja kujitokeza na kudai kuwa ana mtoto katika  familia  ya  aliyekuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa.

Kupitia ukurasa wa mitandao ya kijamii Fred amesema kwao watoto ni Baraka na neema hivyo ameshangaa kuukosa ukoo mzima kujitambulisha.

Amesema anasikitishwa na Makonda anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua.

“Salaams. Nimesikia mwanamama mmioja akiongea kuwa yeye ni ndugu yetu kule Dar es Salaam. Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha. Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Makonda nimekulea.”Amesema Fred

Mwanamke anayedai ana mtoto wa Lowassa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni