Habari/News

Anayedaiwa kuwa daktari feki akamatwa Muhimbili

Tarehe June 19, 2017

DCrJkTlXkAAmggE

Walinzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), leo wamemkamata mtu mmoja anayedaiwa kujifanya daktari na kuwarubuni wagonjwa.

Mtu huyo, Abdallah Juma (30) alikamatwa katika viunga vya hospitali hiyo akizungumza na ndugu wa wagonjwa waliofika kwa ajili ya kuchangia damu huku akiwa na kifaa cha kupimia mapigo ya moyo kikiwa kinaning’inia shingoni mwake.

Hatahivyo, Juma amedai kuwa alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kumsalimia rafiki yake lakini akashangaa akikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema kukamatwa kwa mtu huyo ni muendelezo wa harakati za kupambana na vishoka katika hospitali hiyo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni