Afya

Daktari afungashiwa virago kwa utoro wa siku 9 Kisarawe

Tarehe October 29, 2017

Daktari afukuzwa kwa ulevi.

Utoro wa siku 9 umepelekea  Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mtakayo Emmanuel Shumbusho kufukuzwa kazi.

Uamzi huo wa kumfuta kazi Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mtakayo Bw. Shumbusho umefikiwa na  Baraza la Madiwani halmashauri ya Kisarawe mkoani Pwani kutokana na makosa ya uzembe, utoro kazini ambapo hajaonekana kazini kwa takaribani siku tisa bila taarifa yoyote kwa mwajiri wake.

Akitoa maamuzi ya kikao cha baraza la madiwani ya kumfukuza kazi mganga huyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamis Dikupatile amesema kwamba wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini mapungufu mengi kutoka kwa mtumishi huyo.

Madiwani wote kwa pamoja walikubaliana na uamzi huo kutokana na uzembe wa daktari huyo katika suala zima la utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi na kusababisha kuibuka kwa usumbufu mkubwa kutokana na kutopatiwa matibabu kwa wakati.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni