Habari/News

CUF Z’bar yawataka vijana kujihadhari na matukio ya utekaji

Tarehe April 28, 2018

Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana ya Chama cha wananchi CUF Jimbo la Tumbe Nd. Mohd Nassor Suleiman amewataka wanachama na wananchi kuwa na tahadhari katika maeneo yao kufuatia kuripotiwa kutekwa vijana 6 wa CUF huko  Mtambwe hivi karibuni.

Akizungumza na vijana wa chama hicho huko katika ukumbi wa Bi Awena Hool Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa Wa Kaskazini Pemba  amesema ni vyema kila mmoja kuwa na tahadhari kwani tukio hilo linaonesha taswira mbaya hasa kwa hali ya kisiasa ilivyo hapa nchi.

Amesema  ipo haja kila mmoja kuwa na tahadhari na kuwa makini wakati wa utekelezaji wa majukumu yake yakila siku.

“Vijana tunakuwa wahanga wakuu katika mambo mbali mbali nakuombeni tukitembea tukiwa kwenye kazi zetu tuweni makini tusije tukajikuta tunaingia katika dimbwi hatarishi”. Amesema Nassor

Aidha amewataka vija na wananchi kwa ujumla kuweza kujilinda na kujihami pale ambapo itajitokeza hali ya sintofaham ili kuweza kujinusuru maisha yao.

”Nichukue nafasi hii kukutahadharisheni vijana na wanachi kwa ujumla tuweni na tahadhari kwa pale ambapo utaona kuna hali isiyo yakwaida, tujikinge na mambo yasiyo yalazima kujiepusha na mambo maovu”.Amesema Nassor

Hatahivyo amesema serekali inawajibu mkubwa wa kuwalinda wananchi wake bila kujali itikadi ya chama chake cha kisiasa, dini, kabila hatarangi ilimradi kuweza kutimiza wajibu wake kwa wananchi wote. Sambamba nahayo ameliomba jeshi la polisi kuchukua hatua za madhubuti pale panapo jitokeza vitendo ukiukwaji wa haki za kibinaadamu kama vilivyo fanywa na watu wasio julikana kwa vijana 6 wa mtabwe.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni