Habari/News

CUF yafunguka Sheikh Ponda kuvunja ukimya kuhusu Lissu

Tarehe October 12, 2017

Chama cha Wananchi CUF.

Wakati Sheikh Ponda  akitakiwa kuripoti Polisi kwa madai ya kutoa kauli ya kichochezi,Chama cha Wananchi CUF kimempongeza kwa kuvunja ukimya na kuwataka wananchi kushikamana kutetea  kulindwa kwa haki za binadamu, uhuru wa Kidemokrasia na utawala wa sheria.

Mara baada ya kumtembelea  Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu jijini Nairobi anakopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mnamo Septemba 7, 2017 mjini Dodoma, Sheikh Ponda  amesema  Watanzania bila kujali itikadi zao na imani zao za dini kwa pamoja  wanatakiwa kuungana kutetea haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.

Aidha Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Mbarala Mharagande  amesema  wanampongeza kiongozi huyo kwa uthubutu wake wa kusema ukweli na kukemea maovu mbalimbali ambayo yanaendelea nchini.

“Tunampongeza kwa kujitokeza katika kipindi hiki ambacho Watanzania na Viongozi wengi wa dini na kisiasa wamejazwa woga, wale waliokuwa mstari wa mbele kukemea maovu katika awamu zilizopita hivi sasa wamejitia upofu, ububu na uziwi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari,  amesema kwamba Sheikh Issa Ponda anatakiwa kujisalimisha Polisi  la sivyo hatakua salama.

Amesema  Ponda  ametenda makosa ya jinai kama uchochezi, lakini pia amekuwa anatoa lugha ambazo ni za kejeli, dhidi ya serikali.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni