Habari/News

Chadema watuhumiana kwa usaliti,Katibu akipigwa stop

Tarehe September 27, 2017

Chama cha Chadema

Bundi ametua ndani ya chama cha na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia madiwani sita wa Halmashauri ya Moshi, kutakiwa kujieleza kwa usaliti.

Kufuatia tuhuma hizo Katibu wa Chadema Wilaya ya Moshi, Emmanuel Mlaki amewaandikia barua madiwani hao  akiwataka kujieleza hata hivyo barua hizo zimefutwa na yeye mwenyewe akitakiwa  kusimama shughuli za uongozi ndani ya chama hicho.

Madiwani hao akiwamo Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila walitakiwa kujieleza kwa madai ya usaliti kwa kumchagua makamu mwenyekiti wa halmashauri kutoka NCCR-Mageuzi.

Kwa upande wake  Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema imesema barua zilizoandikwa na Mlaki ni batili na ameagiza ziondolewe katika rekodi za chama hicho.

“Tunautangazia pia umma kuwa Emmanuel Mlaki amesimamishwa uongozi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake na tunautaka umma kusitisha mawasiliano rasmi ya chama kupitia kwake.”Alisema Lema

Chadema na NCCR-Mageuzi ni vyama washirika ndani ya  Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unajumuisha CUF na NLD.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni