Habari/News

CHADEMA kumtoa mbunge wao gerezani

Tarehe January 12, 2017

Cohi-DmUIAAKC8c

Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema kuwa chama hicho kitakata rufaa dhidi ya hukumu ya kwenda jela miezi sita ya Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mheshimiwa Peter Lijualikali wa CHADEMA, iliyotolewa jana na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.

Lissu amesema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio nchini na kudai kwamba, hukumu hiyo ni mwendelezo wa dhuluma dhidi ya wapinzani nchini.

Amesema CHADEMA, pia itamwekea dhamana mbunge huyo ya kuwa nje wakati rufaa hiyo ikishughulikiwa.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni