Habari/News

CCM yaonya wanaopanga safu za Wagombea Urais 2020

Tarehe June 18, 2017

Rais Dkt.John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu.

Rais Dkt.John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu.

Hivisasa,

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa onyo kwa  Makatibu wa chama hicho kuanzia ngazi ya Mashina hadi Taifa wanaoendelea kukisaliti chama hicho kwa kupanga safu za wagombea kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020.

Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula ambapo  amesema chama hicho hakitawavumilia na hawatasita kuwavua uanachama makatibu watakaobanika kufanya usaliti na kupanga safu za wagombea katika chaguzi ndogo zinazoendelea ndani ya chama hicho.

“Bado kuna baadhi ya makatibu wa ngazi ya shina hadi taifa wanaendelea kupanga safu katika chaguzi zinazoendelea, hawa tutawashughulikia,”  amesena Mangula.

Mangula ameongeza kuwa makatibu watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa kanuni za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufukuzwa ndani ya chama.

 

Chama cha Mapinduzi kimewahi kutoa onyo kwa makada mbalimbali waliojitangaza kuwania urais kabla ya muda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika 2015 wakiwemo Edward Lowassa, Bernad Membe pamoja na Januari Makamba.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni