Afya

Bungeni:Upimaji ukimwi na TB sasa kufanyika kwenye Bar

Tarehe April 23, 2018

Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kufanya upimaji wa magonjwa ya virusi vya UKIMWI pamoja na TB kwenye bar.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile leo Aprili 23, 2018 Bungeni jijini Dodoma kwenye kikao cha 15 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema hayo  wakati akijibu la nyongeza kutoka kwa Mbunge Masoud Abdallah aliyetaka kufahamu serikali ina mikakati gani katika kutoa elimu maalum ambayo itaweza kuenea kwa kasi zaidi katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi zaidi.

“Serikali baada ya kuona kumekuwa na changamoto kubwa sana katika utambuzi wa makundi maalum ambayo wengi wamekuwa wakiathirika na ugonjwa wa TB na UKIMWI. Hivyo tumeamua kujielekeza kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari lakini vilevile tuna mkakati mahususi wa kuwatafuta wagonjwa wa TB katika migodi sambamba na hilo tumetengeneza tumetengeneza mikakati jumuishi.”Amesema Ndugulile

“Sasa hivi tumeanza kujielekeza mahali kwenye watu wengi ili tuweze kuwapata kwa pamoja hususani wanaume ambapo mara nyingi wanakuwa katika bar. Msishangae kutuona na sisi tunapita huko kuwaomba kufanya upimaji wa suala la ugonjwa wa UKIMWI pamoja na TB”Amesisitiza Ndugulile.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni