Afya

Bungeni:Serikali kutoa Ajira 25,000 kada ya Afya

Tarehe April 23, 2018

Baadhi ya wahudumu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hivisasa,Dodoma

Watumishi wa kada ya afya wapatao 25,000 wataajirwa Serikalini  katika mwaka wa fedha 2018/19.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kandege wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Mjini, Zacharia Issay (CCM).

Mbunge Issay alitaka kujua mkakati wa Serikali kuhusu kuongeza watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu.

Josephat  amesema Tamisemi imeomba kibali cha kuajiri watumishi wa kada ya afya 25,000 ili kuhakikisha kunakuwapo na watumishi wenye sifa stahiki kwenye hospitali, vituo vyote vya afya na zahanati.

Kwa sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa vituo vya afya 208 nchi nzima ili kuboresha huduna ya dharura kwa mama wajawazito, ujenzi wa vituo hivyo utagharimu Sh bilioni 132.9 hadi kukamilika.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni