Habari/News

Bungeni:Msigwa aibua ufisadi Pasipoti za kielektroniki

Tarehe February 10, 2018

Mbunge wa Iringa Mch Peter Msigwa.

Mbunge wa Iringa  Mch Peter Msigwa amesema ana taarifa za kutosha juu ya ufisadi uliofanyika katika mradi uliozinduliwa na Rais Magufuli hivi karibuni na kudai kuwa Kambi ya Upinzani bungeni wanazo nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka kuhusu namna ufisadi ulivyofanyika.

Msigwa alisema  hayo Bungeni na kuongeza kuwa Serikali imekua  inajipambanua kupambana na ufisadi wakati kuna vitendo vya ufisadi vikiendelea nchini.

Kufuatia kauli hiyo Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson Mwansasu alimtaka Msigwa akatoe ushahidi wake wa namna ufisadi ulivyofanyika kwenye mradi wa mfumo wa uhamiaji mtandao (E-Immigration) kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mhe. Msigwa taarifa ulizonazo kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye hili zoezi zipelekwe kwenye hii kamati, Kamati itakuja kulishauri bunge tufanye nini na huo ufisadi unaoendelea hayo maeneo kwa hiyo naiagiza kamati imuite Mhe. Peter Msigwa na yeye namuagiza Mhe. Msigwa apeleke huko hizo nyaraka ili bunge liweze kushauriwa na kuchukua hatua mahususi” alisema Tulia Ackson.

Mfumo huo mpya  ulizinduliwa na Rais Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli  Januari 31, 2018.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni