Habari/News

Bungeni:Mbunge CCM ahoji Watumishi kuichafua Serikali

Tarehe April 13, 2018

Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby.

Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby amehoji kwa nini  taasisi za serikali zimekua  na tabia ya kutumia Waandishi kuwaita na kuwahoji watu wanaokosoa Serikali.

Akizungumza Bungeni Shabiby amesema kitendo cha Uhamiaji kumuita Mwenyekiti wa TSNP ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu (UDSM), Abdul Nondo na kuhoji uraia wake ni kitendo kinachoichafua serikali ya CCM kwa kiasi kikubwa.

“Kuna watu kwenye Utumishi ambao wanafanya mambo ya kuichafua Serikali ya CCM, kulikuwa na haja gani ya kumita yule kijana Abdul Nondo kumhoji sijui alete cheti cha kuzaliwa cha bibi cheti cha mjomba, cheti cha babu? Mamlaka inashindwaje kufanya investigations zake (uchunguzi) ili kubaini ukweli mapaka iite wanahabari?Amehoji Shabiby.

Amesema kuna watu wengine watatumia hiyo fulsa kusema Serikali ya CCM ikimtaka mtu inamuomba uraia wake.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni