Habari/News

Bungeni:Mbunge CCM ahoji Polisi kutoza faini Madereva

Tarehe April 3, 2018

Mbunge wa CCM Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga.

Mbunge wa CCM Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga ametaka kusikia tamko la serikali kuhusiana na faini zinazotozwa na Askari wa barabarani pindi wanapowakamata madereva wa magari badala ya kuwapa elimu elekezi.

Akijibu swali hilo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema Polisi wamekua wakitoza faini pale wanapobaini kuwa kuna uzembe mwingi barabarani na kuongeza kuwa kama watanzania watazingatia na kuwa waangalifu kwamba wamebeba dhamana kubwa ya maisha ya wenzao Polisi hawatatoza fedha.

“Nitoe rai kwa Jeshi la Polisi kuendelea kuwa wakali pindi watu wanapofanya mzaha, huku wakiwa wamebeba abiria ili kuokoa maisha yanayotokana na ajali nyingi zinazotokea barabarani, na jambo hili ninalo lisemea ni kwa vyombo vya moto vyote kuanzia magari ya abiria na binafsi pamoja na bodaboda. Nalisisitiza hili kwasababu tumeshuhudia vifo vikiwa vimetokea pindi tunapoenda katika eneo la tukio unakuta gari limekwisha andikiwa faini kutokana na kutembea mwendokasi”.Amesema Nchemba

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni