Habari/News

Bungeni: Zitto ahoji Serikali ya JPM Kujitoa ‘OGP’

Tarehe November 13, 2017

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe.

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amehoji kwanini serikali imejitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji serikali kwa uwazi (OGP).

Akizjibu swali hilo waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mh. George Mkuchika amesema baada ya serikali kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, ambapo ameongeza kuwa sio nchi ya kwanza kujitoa kwenye mpango huo.

Aidha,  Serikali ilijiunga  katika Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi (OGP)  Septemba 21 mwaka 2011.

Zitto ameshauri kuwa serikali ingeendelea kuwa mwanachama wa (OGP) ingefaidika kwa sulaa la ndege za Bombadier ambazo zimekwama nchini Canada kutoka na nchi huyo kuwa ndiyo mwenyekiti wa sasa wa OGP.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ndiye aliyezindua  Mpango wa kuendesha serikali kwa uwazi  Septemba 20 mwaka 2011 ukiwa na nchi wanachama 70 Afrika ikiwa na nchi 10.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni