Habari/News

Bunge Lang’aka kukamatwa Mwandishi aliyeripoti ubadhilifu Jeshi la Polisi

Tarehe October 25, 2017

Bunge la Tanzania

Bunge la Tanzania kupitia Kamati ya Hesabu za Serikali PAC limeonesha kukerwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kumkamata na kumuhoji kwa zaidi ya saa tatu mwandishi wa habari  Augusta Njoji wa mkoani Dodoma kwa kuripoti habari iliyotolewa na kamati hiyo kuhusu ubadhilifu uliofanywa na  jeshi hilo.

Kwa mujibu wa tamko la kamati hiyo kupitia Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nagenjwa Kaboyoka, amesema kitendo kilichofanywa na jeshi hilo ni kukiuka kanuni na taratibu za muhimili huo wa bunge kwani suala la waaandishi kuingia kwenye kamati za bunge lipo katika kanuni za bunge.

Inadaiwa kuwa Mwandishi huyo aliripoti habari iliyohusu ubadhilifu katika mikataba ya manunuzi magari ya washawasha ambapo jeshi la polisi limehojiwa na kamati hiyo Oktoba 19 mwaka huu.

“Tunapoona Muhimili mmoja unapoingilia muhimili mwingine kwa nia ya kuficha taarifa ambazo sizo za siri, tunaona kitendo kile ni cha kufanya waandishi wa habari au Kamati ya Bunge ni kulifanya Bunge lisiwe na sauti, kitendo hiki tunakilaani na tunakataa kwamba yoyote mwenye nia ovu ya kutaka kulinyamazisha Bunge au kamati zilizopewa kazi na bunge havitakubalika na tunataka mamlaka husika ichukue hatua kwa kuona kwamba kitendo hicho sicho kitendo halali” AlisemaKaboyoka

Kufuatia kukamatwa na kuhojiwa,Mwandishi Augusta Njoji amesema ameshangazwa na tukio hilo kwani yeye alikuwa akitekeleza majukumu yake kama kawaida na hakuwa na kosa lolote.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto, amesema kesi hiyo imefutwa kutokana na mwandishi huyo hakuwa na sababu ya kuhojiwa.

Vitendo vya kuminya uhuru wa habari vinadaiwa kushamiri nchini siku hadi hadi hivyo pasipokuwa na jitihada za dhati kukabiliana na masuala hayo huenda maisha ya Waandishi na uhuru wa kupata  habari vikawa mashakani.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni