Habari/News

Askofu Shoo awajibu wanaoponda Waraka wa Maaskofu,Asema ni wajinga

Tarehe April 1, 2018

Askofu Dk Fredrick Shoo.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo amewajibu watu wanaoponda  waraka wa Maaskofu kwa kuupaka matope amesema watu hao ni wajinga.

Akizungumza katik  ibada ya  Pasaka leo  katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini, mkoani Kilimanjaro Askofu Shoo amesema kumekuwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa ambao wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kupotosha waraka  wa maaskofu hao na kulipaka kanisa matope kwa malengo yao binafsi jambo ambalo halipendezi na kwamba watu hao ni wajinga.

“Kanisa linasitikika sana, tunaposema jambo la kweli na jambo linalohusu maisha ya Watanzania wote, halafu kunatokea watu chache ambao naweza kuwaita wajinga wanakebehi na kusema eti kwa sababu sadaka zimepungua kanisani sisi sadaka hazijapungua kwani wakristo wanajitoa sana na hatujapungukiwa na kitu ila tunasema yale tunayoyaamini,” amesema.

Askofu Shoo amesema anafahamu kuwa kupitia waraka ule maaskofu wa kanisa hilo watabatizwa majina ya aina mbalimbali na kwamba hizo ni jitihada za kujaribu kuuzima ukweli ulipo katika watara huo na wao hawajali kuhusu hilo bali watasimamia ukweli zaidi.

Katika Waraka wa Maaskofu walidai kuwa wanasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni