Habari/News

Askofu awaasa Viongozi kutofautisha dini na siasa

Tarehe April 2, 2018

Askofu Kiongozi wa Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi Alinikisa Cheyo.

Askofu Kiongozi wa  Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi Alinikisa Cheyo, amewaasa Viongozi wa dini nchini kutofautisha dini na siasa ili kujenga upendo miongoni mwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha amani ya nchi.

Akizungumza kwenye ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Mbeya Mjini Cheyo amewataka watanzania kuacha  kulalamika badala yake wajikite katika kufanya kazi njema inayompendeza Mungu.

Amesema ili  Watanzania waweze  kujiletea maendeleo yenye tija kufikia uchumi wa kati wanapaswa kuachana kulalamika na kujikita   kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni