Habari/News

Agongwa na treni na kufariki akijipiga ‘selfie’

Tarehe February 12, 2018

Mwanamke mmoja amefariki akipiga picha aina ya Selfie na rafikiye katika barabara ya treni nchini Thailand.

Rafikiye alisema kuwa walikuwa wamekunywa pombe na kuamua kujipiga picha hiyo na treni lakini hawakuona treni nyengine iliokuwa ikija kutoka barabara nyengine ya treni, kwa mujibu wa polisi.

Aidha, Miguu yake ilikatika na kufariki hospitalini ambako alikuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi.

Hadi sasa  idadi ya watu wanaofariki wakipiga selfie katika maeneo hatari inaongezeka.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni