Habari/News

ACT-Wazalendo wafunguka kauli ya Baraza la Maaskofu Tanzania

Tarehe February 13, 2018

Chama cha ACT-Wazalendo kimewapongeza Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa kujitokeza mbele na kuongea ukweli kuhusiana na kuminywa kwa Demokrasia nchini bila ya wasi wasi wowote.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu wakatu alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari  katika makao makuu ya ofisi zao amesema hatua ya TEC kutoa waraka wa kiuchungaji ni kurasa mpya katika siasa zetu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ukamilike.

“Tunawapongeza sana viongozi wetu wa dini kwa kujitokeza waziwazi kuonyesha ugandamizaji wa haki unaoendelea nchini. Hatua ya TEC kutoa waraka wa kiuchungaji ni kurasa mpya katika siasa zetu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ukamilike”, amesema Shaibu.

Hivi karibuni Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lilitoa ujumbe huo ndani ya mwezi Februari ,2018 ambapo uliandikwa na maaskofu wote wa baraza hilo ikiwa ni maandalizi ya  mfungo wa mwezi wa toba (kwaresma).

Huu ndio  ujumbe wa Kwaresma wa mwaka 2018.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni