Habari/News

Binti mdogo afukuliwa akiwa hai kifusini

Tarehe September 21, 2017

Mtoto mmoja amegundulika kuwa hai baada ya harakati za waokoaji kuendelea katika nchi ya Mexico ambapo tetemeko kubwa la ardhi limeikumba kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja.

Mtoto huyo amegunduliwa katika kifusi cha jengo la shule, hivyo waokoaji wanajaribu kumfikia mtoto huyo aliyefukiwa na kifusi pindi tetemeko lilipotokea jana.

Aidha waokoaji wamekuwa wakijaribu kumpitishia chakula na maji ndani ya kifusi wakati taratibu zikiendelea ili atoke salama.

Watoto 21 waliepoteza maisha baada ya jengo walilokuwemo kuvunjika huku wengine wakiwa bado ya kifusi hicho .

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni