Habari/News

11 mbaroni kwa kumchapa mwanamke hadharani, sababu yabainishwa

Tarehe January 10, 2017

andrew-satta

Jeshi la Polisi Kanda Maaalum ya Tarime, Mkoani Mara limefanikiwa kukamata watu 11 wote wakazi wa Kinesi Wilayani Rorya kwa tuhuma za kumkamata na kumchapa viboko hadharani mwanamke mmoja mkazi wa kijiji hicho kwa madai ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya mama yake mzazi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Tarime, Kamishna Msaidizi ACP Andrew Satta amesema mwanamke huyo alitandikwa viboko na wajumbe wa baraza la mila la kabila la Wasimbiti jamii ya Wakurya kufuatia malalamiko yaliyopelekwa katika baraza hilo na mama mzazi wa mwanamke huyo.

Amesema tayari watu 11 wakiwemo wazee na viongozi wa baraza hilo wametiwa mbaroni kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha, ameiasa jamii katika kanda hiyo kuacha maramoja vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kufuata mkondo wa sheria unavyosema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni