Burudani/Entertainment

Said Fella amaliza utata kuhusu Radio na TV Station ya Diamond

Tarehe January 12, 2018

Nyumba inayotajwa na tv station ya Diamond.

Meneja wa Diamond, Said Fela amesema Kampuni ya Wasafi Classic (WCB), inayomilikiwa na msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ wanatarajia kufungua televisheni na redio Februari mwaka huu.

Amesema hatua waliofikia ni katika harakati za kampuni hiyo kuendelea kujitanua na kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi.

Ameongeza kuwa   pamoja na kwamba wao ni watu wanaojishughulisha na kazi za burudani, lakini TV yao na redio zitakuwa zinarusha vipindi vya aina zote vikiwemo vya kuelimisha na habari kama vilivyo vituo vingine.

Haya yamebainika ikiwa ni saa chache tangu Diamond na viongozi wa kampuni hiyo watupie jumba la kifahari  ambalo linaelezwa  litakuwa ndiyo  makao makuu ya WCB ambapo mbali ya kuwa na studio za kurekodia muziki pia litakuwa na Redio na TV.

Kuhusu wafanyakazi Fella amesema wameamua kutumia wataalam ambao walikuwa kwenye fani hiyo ikiwemo wazee waliostaafu katika Shirika la Utangazaji(TBC) enzi hizo TVT.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni