Burudani/Entertainment

Rose Muhando awajibu wanaomponda kuhamia CCM

Tarehe December 25, 2017

Mwanamuziki wa Injili Rose Muhando.

Mwanamuziki wa Injili Rose Muhando amewatolea uvivu watu wanaomponda kwa uamuzi wake wa kujiunga na Chama cha Mapinduzi  CCM.

Rose Muhando amesema wanaomponda na kumkebehi anawachukulia ni watu wa kawaida kwani hawezi kujifunza kwa watu walioshindwa huku akidai ameshazoea kusemwa.

“Watu wengine hawaelewagi nini wanachoongea, wanaongea ili waonekane nao wanaongea. Mimi ni mtu ambaye ninayejitambua sawa eehhh!! mimi hata sijali, nimeshazoea kutukanwa kwahiyo hata sihangaikagi na maneno yao.” Amesema Rose

Rose Muhando  na kundi lake la muziki walijiunga na Chama cha Mapinduzi mjini Dodoma kwenye Mkutano Mkuu na kupokelewa na Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni