Burudani/Entertainment

Roma Mkatoliki ageukia Siasa,kugombea ubunge 2020

Tarehe June 17, 2017

Mwanamuziki Roma Mkatoliki.

Mwanamuziki Roma Mkatoliki.

Msanii  wa muziki wa hip hop nchini Tanzania Roma Mkatoliki aliyetamba kwa njimbo za kisiasa  kama mathematics,Tanzania, na KKK amefunguka na kuweka wazi nia yake ya kugombea ubunge.

Akiongea na kituo kimoja cha radio, Roma amesema anajipanga kwa sasa ili aweze kugombea ubunge katika uchaguzi wa 2020.

“Watu wanashauku ya kujua ni chama gani  na jimbo gani nitagombea wasiwe na presha muda ukifika nitaweka wazi zaidi ” Alisema  Roma

Hadi sasa wasanii walioweza kushinda Ubunge ni pamoja na Joseph Mbilinyi (Mr Sugu) Mbeya mjini pamoja na Joseph Haule (Professa J) jimbo la mikumi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni