Burudani/Entertainment

Mwakyembe amteua Alberto Msando kupitia sheria ya Hakimiliki

Tarehe October 26, 2017

Wakili Albert Msando

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe leo amemteua Mwanasheria Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi Leah Kihimbi imesema uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.

Kufuatia uteuzi huo Alberto Msando kupitia ukurasa wake wa Instagram ameahidi kuhakikisha kuwa  sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni