Burudani/Entertainment

Mboto atoa ya Moyoni soko la filamu kuwakatisha tamaa Wasanii

Tarehe June 16, 2017

Msanii wa Filamu za Vichekesho Mboto Haji.

Msanii wa Filamu za Vichekesho Mboto Haji.

Msanii wa filamu za vichekesho nchini Tanzania Mboto Haji amefunguka na kuwapa moyo wasanii wenzake wa filamu waliokata tamaa.

Mboto amesema hayo ikiwa ni maadhimisho  ya siku yake ya kuzaliwa ambapo amesema Wasanii hawana budi kuunganisha nguvu ili kuirudisha bongo Muvi iliyopotea.

“Tunajua soko limeshuka lakini hatuna budi kupambana ili kuweza kulirudisha katika hali yake ya awali kwani bado watanzania wanatuitaji”

Kwa sasa Wasanii wengi wa filamu wamekataa tamaa ya kuendelea na uigizaji kutokana na soko lao kuyumba huku wengine wakikimbilia katika muziki.

“Sanaa yetu inaitaji jitihada na maarifa hivyo kuiacha izidi kudididmia tunaipoteza pasipo kukusudia chonde chonde wasanii wenzangu tusimame na kazi yetu” ameongeza mboto.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni