Burudani/Entertainment

Mama Kanumba atoa ya Moyoni Lulu kutoka Gerezani

Tarehe May 15, 2018

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael ‘Lulu ‘akiwa na mama Kanumba ‘.

Mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema ameumia sana  alipopata taarifa za kuachiwa muigizaji Elizabeth Michael ’Lulu’.

Mama Kanumba amesema, tangu alipopata tetesi za msanii huyo ametoka jela, amejikuta anakosa usingizi na kuumwa presha.

Ameongeza na kusema, kutokana na suala hilo, imemlazimu jana Jumatatu kwenda kwenye maombi kwa ajili ya afya yake hiyo.

“ Lulu alipaswa kukaa hata mwaka mmoja ili roho yake iridhike lakini ndio hivyo,Siku zote maskini hana haki.”Amesema Mama Kanumba

Kwa mujibu wa Jeshi la Magereza kupitia Ofisa Habari wake, Lucas Mboje, alimesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni