Burudani/Entertainment

Hukumu ya Lulu leo mauaji ya Kanumba

Tarehe November 13, 2017

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili Muigizaji wa Filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Hukumu ya Lulu inakuja baada ya baraza la wazee na washauri watatu wa mahakama hiyo kudai kuwa mshtakiwa huyo aliua bila ya kukusudia, Oktoba 27, mwaka huu.

Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya aliyekuwa Muigizaji nguli wa filamu, Steven Kanumba.

Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2010 nyumbani kwa marehemu eneo la Sinza Vatican, Jijini Dar es Salaam.

Mpendwa msomaji kuwa nasi kwa ajili ya kufahamu yale yatakayojiri mahakamani katika hukumu hiyo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni