Burudani/Entertainment

Lipsticks za Wema zapigwa ‘stop’

Tarehe November 11, 2017

Serikali imedaiwa kuzifungia rangi za midomo ‘lipsticks’ aina ya ‘KISS’ zinazozalishwa na Muigizaji Wema Sepetu na kuagiza kutosambazwa kwa rangi hizo kwa madai ya kutokidhi vigezo vinavyotakiwa.

Uamuzi huo unadaiwa kutolewa na Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) baada ya kubaini kuwa rangi hizo hazina ubora kwa matumizi ya binadamu.

Wema ambaye aliwahi kuwa mshindi wa taji la Miss Tanzania alizindua bidhaa yake hiyo ya lipstick mwaka 2015 katika siku yake ya kuzaliwa ambapo pia alijizawadia gari aina ya Range Rover.

Hatahivyo juhudi za kumpata Wema kuthibitisha taarifa hizi hazijazaa matunda huku bidhaa hizo zikiwa zimeadimika kwa muda mrefu katika maduka mbalimbali ya urembo Jijini Dar es Salaam.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni