Burudani/Entertainment

Kauli ya Jay Moe kuhusu kusajiliwa WCB

Tarehe June 16, 2017

Mwanamuziki mkongwe Juma Mchopanga 'Jay Moe'

Mwanamuziki mkongwe Juma Mchopanga ‘Jay Moe’

Msanii mkongwe nchini Tanzania  Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ amekanusha vikali uvumi unaoenea katika mitandao ya kijamii kwamba amesainiwa katika lebo ya WCB.

Akiongea kupitia ukurasa wake wa Instagram,Jay amesema anaheshimu lebo ya WCB pia hajawahi itwa wala kwenda kuomba kujiunga na lebo HIYO hivyo uvumi unaoenea katika mitandao hauna tija kwake.

“Sijawahi sema wala kuandika kujiunga na lebo ya Wcb kwani nilipo ni sahihi na nafanya vizuri naomba sana wanaopenda kusambaza udaku usio na tija wanitafute kabla hawajafanya hivyo niweze kuwaleza”

Lebo ya WCB iliyo chini Diamond ndiyo lebo kubwa kwa sasa na inayofanya muziki mzuri kwenye tasnia ya muziki ya Muziki wa Bongo Fleva.

Baadhi ya Wasanii waliojiunga na WCB ni pamoja  na Lavalava ,Rayvann, Rich mavoko,Harmonize  na wengine.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni