Burudani/Entertainment

Kalapina ataka waliomteka Roma wakamteke na yeye

Tarehe June 18, 2017

Mwanamuziki wa Hip hop nchini Tanzania, Kalapina

Mwanamuziki wa Hip hop nchini Tanzania, Kalapina

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Kalapina ametoa pole nyingi kwa Msanii mwenzake Roma Mkatoliki na wenzake kwa kutekwa hivi karibuni na kumlaumu kidogo kwa kusema kuwa angekuwa ni yeye asingekubali kirahisirahisi kubebwa na kuibgizwa kwenye gari.

Kalapina ambaye anachukuliwa kuwa ni Mbabe kama siyo Mtemi na Ngumi Jiwe amesema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio nchini.

“Nakuambia mimi nina hamu sana na hao watekaji siku wakosee tu waje waniteke mimi kisha wajue kuwa kuna watu tumebarikiwa kwa Ukorofi na Ukorofi tunaujua. Mimi wakija kama 10 na kutaka kuniteka basi nakuhakikishia lazima wakati wanafanikiwa kuniingiza katika Gari lao na kuniteka basi tayari name huku nyuma nitakuwa nimeshawaua. Watatu au Wanne huku waliobaki nikiwaachia maumivu ya kutukuka kabisa. Mdogo wangu Roma ulilegea sana na siku nyingine usifanye hivyo ukiona mtu anataka kukuteka au ana nia mbaya nawe usimcheleweshe na badala yake mpe kipondo,” amesema Kalapina ambaye ni mwanaharakati anayepambana na madawa ya kulevya kwa vijana.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni