Burudani/Entertainment

Bongo muvi watofautiana Wamachinga kukamatwa Kariakoo

Tarehe November 14, 2017

Jimmy Mafufu Msanii wa Filamu Nchini Tanzania

Makamu Mwenyekiti wa chama cha waigizaji Tanzania na Muigizaji mkongwe wa Filamu nchini Jimmy mafufu amekiri kuwa wamachinga wanaojihusisha na uuzaji wa Filamu Kariakoo bado sio tatizo kwa wasanii isipokuwa matatizo yapo na yanafumbiwa macho kwa sababu tu ya uoga.

Akizungumza na mtandao wa Hivisasa amesema wanashangaa kuona mtu kama Msama anasema ameagizwa na Serikali kufukuza watu Kariakoo watu ambao ndio pekee waliobaki kuchukua kazi zao na kuziuza sokoni.

“Sisi tayari tumeshaanza kukaa nao mezani kufanya mazungumzo kuona ni jinsi gani wataziuza kazi zetu, hata mimi najiuliza Serikali ikituma Mamlaka kwenda kubomoa Nyumba za watu waliosogea kwenye hifadhi ya barabara wanawaandaa” Amesema Mafufu

Amesema wao ndio wenye Tasnia na sio Msama hivyo anashangaa kutoshirikishwa katika jambo hilo na imekuwa kama Suprize kwani hajakaa na wao na ni kama amevamia tuu Kariakoo na kutekeleza jambo lao.

Amesema ni vema sasa Mamlaka zikaacha kuhangaika na wauzaji wadogo wadogo ambao wanauza filamu Kariakoo ambao hawana ishu na kama ni Kutafuta Tenda basi itafutwe kwa njia zingine hivyo kuwataka TRA kukaa na wadau bila ya kukurupuka katika kazi.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni