Burudani/Entertainment

Jimmy Mafufu atoa tamko ujio wa Karibu Tandale

Tarehe November 2, 2017

 

Jimmy Mafufu Msanii wa Filamu Nchini Tanzania

Msanii mkongwe wa filamu nchini Tanzania ambaye kwa sasa ni Makamu mwenyekiti wa Chama cha waigizaji Nchini Tanzania Ndugu , Jimmy Mafufu afunguka juu ya ujio wake na filamu mpya ya karibu Tandale

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram Jimmy, Amesema  jiwe walilolikataa wahashi hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni na yeyote litakaye mwangukia litamsaga tikitiki.

“Karibu Tandale ni filamu inayosubiriwa kwa hamu kubwa hivyo mashabiki zangu wajiandae na wakae mkao wa kula mwisho wa mwezi huu wa kumi na moja itakuwa sokoni nchi nzima”

Hapa katikati kulikuwa na upepo wa kushuka kwa soko la filamu nchini Tanzania jambo ambalo limewafanya wasanii kukaa muda mrefu pasipo kuachia kazi mpya.

Ujio wa filamu ya Karibu Tandale unakuletea wakongwe wa Filamu Nchini kama vile Baga Mtemi, Asha Boko na Jimmy Mafufu ambaye ni muandaji wa filamu hiyo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni