Burudani/Entertainment

Harmorapa adai tapeli mnada nyumba za Lugumi ni mtu wake

Tarehe November 11, 2017

Dkt. Luis Shika (mwenye shati na tai)

Msanii anayeongoza kwa kuwa na ‘kiki’ Bongo, Harmorapa ameibuka na kufunguka kuhusiana na mtu aliyeibuka mshindi wa mnada wa nyumba tatu za Mfanyabiashara, Said Lugumi, Dkt. Louis Shika kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 2 lakini akashindwa kutoa asilimia 25 kama inavyotakiwa.

Dkt. Shika ambaye amegonga vichwa vya vyombo vya habari kwa siku mbili zilizopita na kuongelewa midomoni mwa wanajamii aliingia matatani hadi kukamatwa na kuwekwa ndani kufuatia kushindwa kutoa asilimia 25 ya gharama kamili ya nyumba hizo baada ya kubainika kutokuwa na pesa hiyo na kupelekea mnada huo kuharibika.

Kupitia ukurasa wa Instagram unaodaiwa kuwa wake, Harmorapa ameibuka na kudai kuwa mzee huyo aliyebatizwa jina la ‘Tajiri Mtata’ ni baba yake na kwamba anashangaa kusikia amekamatwa.

Huu ni mnada wa pili kukwama katika uuzwaji wa nyumba hizo za Lugumi baada ya mnada wa kwanza kushindikana kutokana na bei ya nyumba hizo kuwa kubwa sana.

Hatahivyo, Jeshi la Polisi limedai kuwa kuna tetesi kuwa mtu huyo alitumwa na Lugumi ili kuvuruga mnada huo wa pili ili nyumba hizo zisiuzwe.

Serikali inazipiga mnada nyumba za Lugumi kutokana na deni analodaiwa mfanyabiashara huyo kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni