Burudani/Entertainment

Hali ya mzee Majuto bado tete

Tarehe April 24, 2018

Mchekeshaji wa filamu za Kibongo , Amri Athuman maarufu Mzee Majuto, amelazwa tena katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa.

Kwa mujibu wa Mke wa mwigizaji huyo, Aisha Yusufu amesema kidonda alichofanyiwa upasuaji kimeleta shida, hivyo kumpeleka kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Majuto alilazwa hospitalini hapo Januari mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa tezi dume.

Mzee Majuto amejipatia umaarufu mkubwa kupitia filamu za uchekeshaji ndani na nje ya nchi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni