Burudani/Entertainment

Gabo aibua mikakati yake kuirudisha Bongo muvi

Tarehe June 16, 2017

Gabo-1

Msanii wa filamu Nchini Tanzania Gabo Zigamba

Msanii wa filamu nchini Tanzania  aliyetamba na filamu Bado Natafuta Gabo Zigamba amewataka watanzania kujua kwamba hakuna stori mpya ambayo wataifanya wasanii wa filamu, kwani stori nyingi zimeshatumika ila wanachokifanya kwa sasa ni kuboresha stori na kuiingiza kwenye uhalisia wa watanzania.

Akiongea na mtandao huu Jumatano hii wakati akizindua filamu yake mpya ya Kisogo, Gabo alidai hakuna kitu kipya ambacho kitafanywa na wasanii wa filamu kikaonekana ni cha kwanza kuonekana au kufanyika duniani.

“Unajua watu wanashindwa kuelewa kwenye ishu za stori zetu za filamu, wanasema stori ni zile zile na wanataka stori mpya wanashindwa kutambua hakuna stori ambayo utaitoa ukasema hii haijawahi kutumika duniani,” alisema Gabo

Kila stori ambayo unaiona kwenye filamu ni stori ambayo tayari iliwahi kutumika sehemu fulani sisi tunachokifanya ni kuboresha wazo na kupata kitu kipya

Muigizaji huyo alisema ameamua kulivalia njuga suala la kuikomboa tasnia ya filamu na kuhakikisha watu wanarudisha imani kwa filamu za ndani.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni