Burudani/Entertainment

Diamond,WCB matatani kwa wizi wa kionjo

Tarehe November 10, 2017

Wasanii wa kundi la WCB.

Mmiliki wa kundi la WCB Diamond pamoja na kundi lake  wametakiwa kulipa fidia ya shilingi za kitanzania milioni 300 kwa wizi wa kionjo  cha muziki uliopigwa katika wimbo wa ‘Ajali’ bila idhini ya mmiliki.

Msondo Ngoma kupitia kampuni ya Mawakili ya Maxim imeitaka Wasafi Clasic Baby (WCB) kuwalipa fidia ya kiasi cha shilingi 300 milioni kutokana na kutumia kionjo hicho cha muziki kilichotungwa na kupigwa katika wimbo wao wa ‘Ajali’ na kukirudia katika wimbo wao wa ‘Zilipendwa’ bila kupata idhini ya mmiliki.

Kionjo hicho kilichotungwa na kupigwa kuanzia dakika ya 6:38 hadi 6:52 kwenye wimbo wa ‘Ajali’ mali ya Msondo Ngoma, kimeigwa na kupigwa katika wimbo wa ‘Zilipendwa’ kuanzia dakika ya 4:55 hadi 5:10.

Kwa mujibu wa Barua hiyo imeitaka WCB kulipa fedha hizo ndani ya muda wa siku saba na kama wakishindwa basi Msondo Ngoma watawachukulia hatua zaidi za kisheria.

Wimbo wa zilipendwa umeangaliwa na watu 9,341,253 tangu ulipowekwa Youtube kupitia akaunti ya Diamond Platnumz.

Wimbo huo umeimbwa na Diamond Platnumz , Rayvanny , Harmonize , Mbosso ,Lavalava na Queen Darleen

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni