Burudani/Entertainment

Diamond kuja na albamu ya 3, ‘A Boy From Tandale’

Tarehe October 12, 2017

Msanii wa Muziki wa Bongoflava na Mshindi wa tuzo ya mwanamuziki bora wa kiume Afrika Mashariki kwa miaka minne mfululizo katika tuzo za Afrimma, Diamond Platnumz ametangaza ujio wa albamu mpya aliyoipa jina la ‘ A Boy From Tandale’.

Mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo mpya wa Hallelujah, amesema yupo kwenye maandalizi ya mwisho kutengeneza kazi hiyo ambayo ni maalumu kwa mashabiki wanaopenda muziki wake.

Ujio wa albamu hiyo unachagizwa zaidi na tukio la Msanii huyo la hivi karibuni baada ya kuonekana akirekodi video na Msanii wa HipHop nchini Marekani, Rick Ross, huku mashabiki wake wengi wakifurahishwa na kudai kuwa sasa msanii huyo amuwa wa kimataifa kiukweli.

Diamond aliutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuwataarifu mashabiki kuhusu kazi hiyo mpya akiandika, “Album soon come, #ABoyFromTandale”.

Inadaiwa kuwa Albamu hiyo ambayo itakuwa ya tatu kwa Platinumz baada ya zile za Kamwambie na Lala Salama, itahusisha baadhi ya nyimbo kama, Number One na Number One Rmx, Nasema Nawe, Bum Bum, Nitampata wapi na Nana.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni