Burudani/Entertainment

Darassa: Jina la ‘Simba’ halimfai Diamond Platinumz

Tarehe January 4, 2017

darassa cmg

Msanii wa HipHop anayetikisa kwa sasa, amesema kuwa msanii mwenzake wa Bongofleva, Daiamond Platinumz hapaswi kujiita Simba kwakuwa yeye ni zaidi ya sifa za mnyama huyo.

Darassa pia ameweka wazi ule mstari wake wa “sio simba, sio chui, sio mamba” kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.

Darasa amesema Diamond ni msanii ambaye amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo mafanikio yake na uwezo wake wa muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama Simba.

“Ningekuwa Diamond nisingejiita simba, ninavyomuona Diamond ni zaidi ya Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana,” amesema Darassa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni