Burudani/Entertainment

Daimond kupagawisha Wakazi wa Zanzibar siku ya Nyerere day

Tarehe October 12, 2017

Nasibu Abdul ‘Daimond’Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nchini Tanzania

Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere huazimishwa kila ifikapo tarehe 14/10 ya kila mwaka.

Akizungumza na wanahabari Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi Mh, Ayuob Mohammed, amesema siku ya kumbukumbu ya mwalimu nyerere itaambatana na maadhimisho ya  kilele cha mwenge wa uhuru.

Mh,Ayoub Mohammed Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi

“Nawaomba wakazi wa Zanzibar na viunga vyake kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Amani siku ya Jumamosi kuweza kushuhudia burudani mbalimbali ”

Siku hiyo itapambwa na Burudani kutoka kwa msanii anayefanya vizuri  kwa sasa Nasibu Abdul ‘Daimond’

Mkuu wa mkoa alitumia fursa hii kuwaomba wakazi wa mkoa wa mjini Magharibi   wasiwe na hofu wala shaka kwani jeshi la polisi limejipanga kusimamia vema Raia pamoja na mali zao.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni