Burudani/Entertainment

Chris Brown, Soulja Boy kuonyeshana Dubai

Tarehe January 11, 2017

chris-brown-soulja-boy-boxing-composite-3-1

Pambano la wakali wawili kati ya Chris Brown na Soulja Boy linatarajiwa kufanyika huko Dubai.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa TMZ, wawili hao wamekubali kupigana kwenye pambano hilo ila wanachotaka ni kupata fedha zaidi kupitia kwa watu ambao watataka kuangalia pambano hilo [Pay-Per-View].

Awali pambano hilo lilipangwa kufanyika mjini Las Vegas lakini kutokana na sheria zilizopo katika mji huo kutokana na mapambano kama hayo ndio imesababisha kubadilishwa kwa ratiba hiyo.

Hata hivyo imedaiwa kuwa pambano hilo litakuwa ni kwa ajili ya kujitolea na fedha zitakazopatikana zitatolewa kama msaada.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni