Burudani/Entertainment

Bongo Movies washikwa mkono na ppf

Tarehe October 12, 2017

Jimmy Mafufu makamu m/Kiti wa chama cha waigizaji Tanzania

 

Baada ya kilio cha muda mrefu cha wasanii wa filamu nchini Tanzania  kilichochangiwa na kuyumba kwa soko la filamu ppf yawashika mkono.

Akizungumza na vyombo vya habari Makamu mwenyekiti wa Chama cha waigizaji nchini Tanzania Jimmy Mafufu amesema umefika wakati wasanii tuache habari ya kudharau masuala mbali mbali yanayojitokeza katika tasnia yetu

“Tunaomba wasanii wote mjitokeze kwa wingi siku ya jumamosi katika viwanja vya Posta Kijitonyama Ili kuweza kujisajiri katika mfuko wa  bima ya afya kwani ni muhimu kwetu na garama nafuu”

Kumekuwa na tabia ya wasanii wa filamu kushindwa  kujikwamua hasa katika matatizo hivyo ni vema kutumia fursa hii iliyotolewa na mfuko wa kijamii wa Ppf ili kuepuka tabia ya kuchangiwa.

Afisa habari wa Chama cha Waigizaji nchini Tanzania Ndugu ‘Chick Mchoma’ ametumia nafasi hii kuwasisitiza wasanii kwamba jambo hili sio la kisiasa.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni