Burudani/Entertainment

Bexy Wamusic atoa ya moyoni Dogo Janja kumuoa Uwoya

Tarehe November 14, 2017

Bexy Wamusic Msanii wa muziki wa Bongo Fleva

Msanii wa Mziki wa Bongo Fleva Nchini Tanzania anayetamba na Ngoma yake Mpya ya Yolanda ametoa ya moyoni  kuhusu  ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya.

Akizungumza na Sasa Tv leo  Bex Wamusic amesema ifike wakati maamuzi ya moyo yasiingiliwe na mtu kwani mapenzi ni jambo la makubaliano ya watu wawili.

“Binafsi siwezi sema chochote juu ya ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya kwani wamependana ndio maana wamefunga pingu za maisha na sio jambo geni maana wapo Wasanii wengine kama Diamond na Zari, Iyobo na Aunt Ezekiel”Amesema Bex.

Ndoa ya Dogo Janja na Irene uwoya imezua gumzo katika mitandao ya kijamii kufuatia Msanii Dogo Janja kutofautiana umri na Mwigizaji wa filamu Bongo Irene Uwoya.

Bexy wa Muziki ametumia fursa hii pia kuwaomba mashabiki zake waendelee kumuunga mkono kwa kuzidi kusapoti kazi zake kwani anaamini hato waangusha.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni