Burudani/Entertainment

Mwakyembe ageukia wasanii nyimbo za injili

Tarehe August 11, 2017

20770213_1550093235034089_4720546931615345850_n

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe amekutana na wasanii wa nyimbo za Injili Jijini Dar es Salaam kusikiliza changamoto zinazoikabili tasnia ya muziki wa nyimbo za injili na kuweka mikakati ya kuzitatua changamoto hizo kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mkutano na wanamuziki wa nyimbo hizo, Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali ina wajibu wa kufuatilia changamoto za tasnia ya muziki ukiwemo muziki wa injili na kuzitatua ili kuweza kukuza kazi za wasanii kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na taifa.

“Muziki ni tasnia ambayo imewabeba vijana wengi hapa nchini, serikali ina wajibu wa kutetea, kulinda na kuhakikisha maslahi ya kazi za sanaa ikiwemo muziki wa injili inaheshimiwa na kulindwa,” amesema Mhe. Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe amekutana na wasanii wa nyimbo za injili siku chache tu baada ya kukutana na wale wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Flava’.

20768031_1550093255034087_6479120320101778323_n

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni