Afya

Wazee waliopigana vita ya Dunia wafichua ‘siri’ ya matibabu bure

Tarehe June 7, 2017

Baadhi ya wazee waliopigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Baadhi ya wazee waliopigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Kutokana na manyanayaso wanayoyapata wakati wanapohitaji matibabu chama cha Askari waliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia(TLC) leo wameiomba Serikali kuunda sheria kuhusu suala la matibabu bure liweze kufahamika kama haki  ya kisheria  na kushughulikia matatizo yao kama wazalendo wa nchi.

Mwenyekiti wa chama hicho Rashid Ngonji alisema licha ya agizo hili bado kuna hali ya sintofahamu kwenye matibabu ya wazee kwani katika badhi ya hospitali wanauliza pesa za matibabu  na bima za afya licha ya kuwepo kwa tamko hilo.

“kwa sasa hali zetu sio nzuri kiuchumi na tunahitaji kusaidiwa ili tuweze kujikwamua  kimaisha” alisema Rashidi.

Kwa sasa Chama hicho kina jumla ya wanajeshi ambao ni wanachama 867.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni